Mkutano

 

Ratiba ya mkutano huu imeandaliwa katika vipengele tofauti vitakavyomwezesha kijana kufwatilia katika mtililiko njia tofauti za kurudisha hadhi ya Afrika. Tumeandaa Mpangilio rahisi wa matukio katika mkutano, utamwezesha mshiriki kuchagua kiurahisi vipindi atakavyopenda kuudhuria katika mkutano.

 

Nguvu

Kipindi cha nguvu kitalenga katika sera ya ushiriki wa vijana na uwezo wa Vijana kujikita kwenye siasa pamoja na taasisi na sera zinazotuongoza.  

Watu

Kipindi cha WATU kitalenga katika masuala ya kijamii na kitamaduni yanayoathiri Vijana.

Kipindi kitatia mkazo juu mambo yanayohusu wakimbizi na uraia,. juu ya wajibu wa viwanda vya ubunifu, ukimwi na Vijana.

Uwezo

Kipindi cha UWEZO  uwezo wa baadaye na fursa ya Vijana kwa Afrika. Kipindi kitalenga juu ya Vijana na ujasiliamali, ajira na mapinduzi ya viwanda.

Mwenyeji wa Mkutano

Mkutano wa Vijana  wa BDBA utafanyika katika jiji kubwa ndani ya Gauteng lijulikanalo kama Johannesburg. Kwa kuweka mkutano kwenye kitovu cha uchumi wa nchi ya Afrika ya Kusini, mkutano upo  sio tu kutoa nafasi kuhamasisha ushiriki lakini pia kuwapa washiriki nafasi ya pekee ya kufikiria kwa umakini jinsi ya kuboresha maisha ya jamii na kuongeza maendeleo kuelekea mabadiliko chanya kwenye nyanja za kijamii, kiuchumi na kanda ambazo zitanufaisha vijana na vizazi kijacho.

Johannesburg ni jiji kubwa na lenye watu wengi nchini Afrika Kusini. Chimbuko lake lilitokana na machimbo ya madini mnamo mwa miaka ya 1800, Johannesburg kwa sasa ni kitovu cha uchumi na biashara nchini Afrika ya Kusini na nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara. Johannesburg inachangia pato la ndani la nchi ya Afrika ya Kusini karibia 16%.  jimbo la Gauteng ambapo jiji la Johannesburg lipo, linajulikana kama moja ya jimbo kubwa kiuchumi na linachangia takribani theruthi ya uchumi wa nchi ya afrika ya kusini. Kutokana na takwimu za 2016 za pato la ndani la jimbo.

Johannesburg nini moja ya sehemu zinazofikika kirahisi ndani ya Afrika. Uwanja wa ndege wa Tambo ndio uwanja mkubwa na wenye shughuli nyingi barani afrika. Unahudumia takribani ndege 50

Agenda