Sisi ni nani

 

The breaking down border initiative ni jukwaa la Vijana linaloongozwa na Vijana wa kiafrika kwa manufaa ya Vijana wa kiafrika. Wazo la kuanzisha harakati  imetiwa hamasa na maono ya kuunganisha Vijana wa kiafrika na kushirikishana ujuzi ili kujenga afrika mpya. BDBA Imewekeza Zaidi katika kukutanisha Vijana wa kiafrika 

Kushiriki pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kuijenga afrika ya ijayo/mpya/ baadaye.

Harakati hizi zinalenga kulishughulikia pengo linalozuia maendeleo  ya Vijana wanaofanya kazi katika mazingira ya kijamii na kiujasiliamali. Hii ni pamoja na:

Wavumbuzi wa Afrika kutokuwa na uwezo wa kutumia vipaji vyao kujenga kazi  na ukosefu wa fursa katika jukwaa la kimataifa hasa la barani afrika.

Vijana kukosa fursa ya kushirikiana na wataalamu na ujuzi nje ya mipaka

Ukosefu wa uwekezaji katika afrika na waafrika.

Changamoto zilizotajwa ndizo zilichangia katika mipango ya harakati :-

 

  • Breaking Down Borders Africa Tour:
    Ilizinduliwa 2016, ziara hii ya BDBA ni mpango wa kubadilishana ulianzishwa kwa kusudi la Vijana kupata fursa ya kushirikiana, utetezi wa upatikanaji wa elimu bora na ujasiliamali kwa Vijana. Pia kutembelea/kujifunza Sanaa, urithi na utalii wa nchi wenyeji.

 

  • The Breaking Down Borders Africa Youth Summit

    mkutano huu unafanyika kwa mwaka mara moja ukiwa na lengo la kukutanisha Vijana walio katika Nyanja mbalimbali kazi na taaluma  kujumuishwa pamoja katika jukwaa ili kubadilishana ujuzi na uzoefu ili kujenga afrika ijayo. Mpaka sasa mkutano umewakutanisha  viongozi Vijana 250 kutoka katika nchi 18 barani Afrika kupiga kasi katika uhamasishaji wa elimu, harakati za kijamii na kisiasa kwa kushirikiana katika maeneo tofauti.

BDBA INITIATIVE kwa kupitia jukwaa Imeimalisha ushirikiano na kukuza uhusiano kati ya Vijana ndani ya afrika na ughaibuni.